pmbet

Mo Salah atarudi kwenye kiwango cha kutupia - Arne Slot

Eric Buyanza

February 27, 2026
Share :

Kocha Arne Slot ana matumaini kuwa Mohamed Salah ataanza kufunga mabao tena hivi karibuni, akisisitiza kwamba hana wasiwasi na ukame wa mabao wa mshambuliaji huyo wa Misri kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.
 

Salah, ambaye ana umri wa miaka 33, hajafunga bao katika mechi 9 za Ligi Kuu, jambo ambalo limesababisha wasiwasi miongoni mwa mashabiki wa Liverpool. Hata hivyo, Slot anaamini kuwa Salah atarudi tena kwenye kiwango chake cha kufunga mabao, akieleza kuwa mshambuliaji huyo wa Misri amewahi kupitia kipindi kigumu kama hicho hapo awali.
 

Slot pia anasema Salah anajua anachopaswa kufanya, na kwamba anahitaji tu kujiamini tena.

 

Kocha huyo wa Liverpool aliwataja wachezaji kama Hugo Ekitike na Cody Gakpo wanaopitia ukame wa mabao, hivyo basi suala hilo si kwa Salah pekee yake
 

Liverpool watawakaribisha West ham United Jumamosi hii kwenye uwanja wa Anfield.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet