Modric aonesha nia ya kusalia Madrid
Eric Buyanza
April 23, 2024
Share :
Kiungo wa kati wa Real Madrid Luka Modric anatamani kuongeza muda wake wa kuitumikia klabu hiyo kwa mwaka mwingine.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38, ambaye kwa sasa yuko katika kipindi cha mwisho cha mkataba wake Santiago Bernabeu, ameonyesha nia ya kuendelea kubaki na wababe hao wa Uhispania licha ya tetesi zinazomhusisha na uwezekano wa kumalizia soka lake Saudi Arabia.
Licha ya umri wake, Modric amekuwa mhimili mkubwa katika kikosi cha Ancelotti, akichangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya hivi karibuni ya timu hiyo.