Modric aweka rekodi mpya Euro, akataa kustaafu
Sisti Herman
June 25, 2024
Share :
Baada ya kufunga goli kwenye mchezo wa raundi ya tatu ya kombe la Mataifa Ulaya (Euro) kundi B, Croatia dhidi ya Italia, Luka Modric amendika historia ya kuwa mchezaji aliyefunga goli akiwa na umri mkubwa zaidi kwenye historia ya michuano hiyo akiwa na miaka 38 na siku 289.
Licha ya kufunga goli hilo sikunde kadhaa baada ya kutoka kukosa mkwaju wa penalti, Croatia haikuweza "kushilikia bomba" kwa dakika zote 90 kwani kwenye muda wa nyongeza sekunde kadhaa kabla ya dakika 8 zilizoongezwa kutamatisha mchezo, Mchezaji aliyetokea benchi dakika ya 81 Mattia Zaccani aliisawazishia goli Italia.
Kwenye mkutano na wanahabari, mwandishi wa Italia alimuomba Modric kutostaafu kama wengi wadhanivyo lakini yeye alimjibu kwakumuambia "huu sio wakati wa kufikiria kustaafu kwake".
Baada ya kupoteza Croatia inategemea miujiza ya kuweza kufuzu kwa kanuni ya timu bora za nafasi ya 3 "Best Looser" wakisubiri matokeo ya timu za nafasi ya 3 za makundi mengine, Italia na Hispania wamefuzu kwenye kundi hilo.