pmbet

Mohamed Salah anataka mkataba wa miaka 3 Ili abakie Anfield

Eric Buyanza

November 29, 2024
Share :

Mohamed Salah anaripotiwa kutaka apewe nyongeza ya kandarasi ya miaka mitatu ili aendelee kubakia Liverpool.

Mshambuliaji huyo wa Misri, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2025 na anaelezwa kujaribu kuwapa shinikizo wamiliki wa klabu hiyo.

Ikiwa Liverpool watakubali kumuongezea mkataba huo basi utamalizika akiwa na umri wa miaka 36.

Kwasasa umebaki mwezi mmoja ili aweze kuwa kwenye nafasi ya kufanya makubaliano ya awali na vilabu vingine vinavyomuhitaji. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet