pmbet

Mohammed Abdulraham wa DW afariki dunia

Sisti Herman

July 16, 2025
Share :

 

Kwa masikitiko makubwa tumepokea taarifa ya kifo cha Mohammed Abdulraham, aliyewahi kuwa manyakazi wa muda mrefu na Naibu Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW - Deutsche Welle.

Marehemu Abdulraham alihudumu kwa zaidi ya miaka 30 akiwa kiungo muhim katika kukuza, kuendeleza, na kuimarisha tasnia ya utangazaji wa Kiswahili katika DW na nje yake. Alijulikana kwa uadilifu, weledi na mchango wake mkubwa kwa waandishi chipukizi na jamii kwa ujumla.

Amekuwa kielelezo cha uandishi wa habari wa kiwango cha juu, na tunamkumbuka kwa mchango wake mkubwa uliogusa
maisha ya wengi.

Tunatoa pole nyingi kwa familia yake, marafiki, wafanyakazi wa sasa na wa zamani wa DW, na wote walioguswa na msiba huu.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet