pmbet

MOI yafanya upasuaji wa Ubongo kwa kutimia AI

Sisti Herman

March 30, 2025
Share :

 

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeanza rasmi upasuaji wa ubongo kwa kutumia kifaa kiitwacho ‘Brain Lab- Neuro Navigation System’ Akili Unde, ambacho husaidia Wataalamu kufanya upasuaji wa ubongo bila kufungua fuvu na kupunguza siku za Mgonjwa kukaa wodini baada ya upasuaji huo.

Akiongea Jijini Dar es salaam March 27,2025 Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema Taasisi ya MOI ndio Hospitali ya kwanza Tanzania kufanya upasuaji wa ubongo kwa kutumia akili unde.

“Kwa mara ya kwanza katika nchi yetu (Tanzania) leo tumefanikiwa kufanya upasuaji wa ubongo kwa kutumia kifaa maalum ( Brain Lab- Neuronavigation System) ambacho kinamuongoza Daktari mpaka kwenye shida ilipo bila kufungua fuvu wala mionzi ya X- Ray”

Dkt. Mpoki amesema kuwa upasuaji huo umeongozwa na Daktari bingwa mbobezi mzawa kwa kushirikiana na Madaktari kutoka Chuo Kikuu cha Weill Cornell cha nchini Marekani na kutoa wito kwa Watanzania wenye matatizo ya ubongo kufika katika Taasisi hiyo kupatiwa matibabu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet