pmbet

Mojtaba Khamenei aidhinisha makubaliano ya kumaliza vita

Eric Buyanza

June 19, 2026
Share :

Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Mojtaba Khamenei, ameunga mkono mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani, katika taarifa iliyosomwa kupitia vyombo vya habari vya serikali.
 

Hiyo ni kauli yake ya kwanza tangu makubaliano hayo kufikiwa, na inaonekana kuashiria mabadiliko ya msimamo wa Iran kuhusu mazungumzo na Marekani. Kiongozi huyo mkuu hajajaonekana hadharani tangu alipojeruhiwa katika shambulio mwanzoni mwa vita.

 

Makubaliano hayo, yaliyotiwa saini na Rais wa Marekani Donald Trump pamoja na Rais wa Iran Masoud Pezeshkian,  yameanzisha kipindi cha siku 60 cha mazungumzo mapana zaidi kati ya nchi hizo mbili, ikiwa ni pamoja na mpango wa nyuklia wa Iran.

Bei za mafuta zilishuka kwa kasi baada ya makubaliano kutiwa saini.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet