Morocco kukata rufaa CAF
Sisti Herman
February 5, 2026
Share :

Morocco iko tayari kukata rufaa dhidi ya uamuzi uliosababisha faini ya dola$415,000 sawa na zaidi ya Shilingi Bilioni 1, na kufungiwa mechi, baada ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2025, shirikisho la soka la nchi hiyo lilithibitisha Jumanne.
Senegal, ambayo ilishinda 1-0 baada ya muda wa ziada, haitapinga uamuzi wa CAF.
Wakati wa fainali hiyo, vijana waokota mipira walijaribu kuchukua taulo kutoka kwa kipa wa Senegal, Edouard Mendy. Tukio hili moja lilisababisha faini ya $200,000 kwa Simba hao wa Milima ya Atlas.
Lakini Waafrika Kaskazini wanaamini adhabu kutoka CAF ilikuwa kali sana.
"Kwa kuzingatia kutolingana kati ya vikwazo hivi na ukubwa na uzito wa matukio, FRMF imeamua kupinga maamuzi haya," shirikisho la soka la Morocco lilisema katika taarifa.





