Morocco yaomba kuandaa AFCON 2028
Sisti Herman
February 12, 2026
Share :

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limethibitisha kupokea zabuni tatu za kuomba 'uenyeji' wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2028.
Morocco, ambayo ilikuwa mwenyeji wa AFCON 2025, imewasilisha maombi ya kuandaa mashindano hayo mwaka 2028. Wakati huo huo, mataifa ya kusini mwa Afrika Botswana na Afrika Kusini yameungana na kuwasilisha zabuni ya pamoja kuwania nafasi hiyo.
Aidha, Ethiopia nayo imewasilisha rasmi maombi yake ya kuomba kuwa mwenyeji wa fainali hizo za mwaka 2028.
Kamati utendaji ya CAF inatarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki hii ili kufanya uamuzi wa mwisho kuhusu nchi itakayopata nafasi ya kuandaa AFCON 2028.
Uamuzi huo unatarajiwa kuwa wa kihistoria na wenye athari kubwa kwa mustakabali wa soka la Afrika.





