pmbet

Morocco yapewa nafasi kuandaa fainali kombe la dunia 2030

Sisti Herman

September 10, 2026
Share :

 

Kinyang’anyiro cha nchi itakayofanikiwa kuandaa mchezo wa Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2030 kimeendelea kushika kasi, huku Morocco na Spain zikitakatika katika mchuano mkali wa kidiplomasia na miundombinu, huku Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) likiwa bado halijatoa uamuzi wa mwisho.

 

Ingawa michuano hiyo mikubwa itashirikisha mataifa matatu wenyeji—Morocco, Spain, na Ureno—macho yote kwa sasa yameelekezwa kwenye uamuzi wa wapi utakapopigwa mchezo huo wa fainali unaosubiriwa kwa hamu kubwa duniani kote.

 

Silaha ya Morocco: Uwanja Mkubwa Zaidi Duniani


Serikali ya Morocco imeweka wazi nia yake ya kuandika historia kwa kujenga uwanja mpya wa kifahari wa Hassan II mjini Casablanca. Uwanja huo unaotarajiwa kuchukua mashabiki 115,000, utakuwa uwanja mkubwa zaidi wa soka duniani pindi utakapokamilika. Morocco inatumia kete hii kama kigezo kikuu cha kuishawishi FIFA kuwa Afrika inastahili kuwa mwenyeji wa fainali hiyo kuu.

 

Spain Yafungua Makucha kwa Historia na Hadhi


Kwa upande mwingine, Spain haiko nyuma ikijivunia miundombinu yake ya kisasa na uzoefu wa muda mrefu. Jiji la Madrid linaupigania uwanja uliokarabatiwa hivi karibuni wa Santiago Bernabéu (wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 83,000), uwanja ambao ulishawahi kuandaa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1982.

 

 Aidha, jiji la Barcelona nalo liko kwenye mbio hizo likiwakilishwa na uwanja mkubwa wa Spotify Camp Nou unaofanyiwa maboresho makubwa kufikia uwezo wa kuchukua mashabiki 105,000.

 

Ureno Yakaa Pembeni, FIFA Yabaki Kimya

 

Wakati mataifa haya mawili yakichuana, nchi ya Ureno imejiondoa rasmi kwenye kuwania fainali hiyo kutokana na viwanja vyake kutofikia vigezo vya ukubwa vinavyohitajika na FIFA kwa mechi ya fainali.

 

Hadi sasa, FIFA imesisitiza kuwa taarifa zote zinazodai nchi fulani imeshabarikiwa kuandaa fainali hiyo si za kweli. Maafisa wa soka kutoka pande zote mbili wanaendelea kushawishi, huku uamuzi rasmi ukitarajiwa kutolewa hapo baadaye baada ya tathmini ya kina ya kamati za ufundi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet