pmbet

MOTO WA HAALAND: Afunga 2 dhidi ya Denmark, avunja rekodi za magwiji

Eric Buyanza

September 25, 2026
Share :

Mshambuliaji hatari wa timu ya taifa ya Norway na klabu ya Manchester City, Erling Haaland, amezidi kuandika historia ya kipekee katika ulimwengu wa soka baada ya kufikisha jumla ya mabao 64 akiwa na kikosi cha timu yake ya taifa.

 

Hatua hiyo imekuja kufuatia kiwango bora alichokionyesha usiku wa kuamkia leo, ambapo alifunga mabao mawili muhimu na kuiongoza Norway kupata ushindi mnono wa mabao 3-2 dhidi ya Denmark katika mfululizo wa michuano ya UEFA Nations League.

 

Haaland amefikia idadi hiyo ya mabao 64 katika michezo 56 pekee aliyoichezea Norway, jambo linalomfanya kuwa na wastani wa juu zaidi wa ufungaji  ikilinganishwa na mchezaji yeyote wa soka wa kizazi cha sasa. Katika mchezo huo wa dabi ya Skandinavia, Haaland alihitaji dakika 18 tu kupachika bao lake la kwanza kabla ya kuongeza la pili kunako dakika ya 74.

 

Mabao hayo yanamfanya kupindua rekodi za magwiji wa soka kama Ronaldo Nazario wa Brazil na Zlatan Ibrahimović wa Sweden, ambao walimaliza soka la kimataifa wakiwa na mabao 62 kila mmoja.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet