Motsepe atinga Kenya kumaliza mgogoro wa FKF
Eric Buyanza
May 11, 2026
Share :

Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Patrice Motsepe anatazamiwa kukutana na maafisa wa ngazi za juu wa shirikisho la soka nchini Kenya (FKF) huku kukiwa na mizozo katika Shirikisho hilo.
Ziara ya Mkuu huyo wa soka Afrika ni sehemu ya Mkutano wa CAF utakaofanyika Nairobi Mei 11-12, 2026.
Rais wa FKF, Hussein Mohammed alitimuliwa na wajumbe wa kamati kuu ya kitaifa (NEC) mwezi uliopita, katika mkutano ulioongozwa na Makamu wake, McDonald Mariga.
Rais anadaiwa kuhusika katika upotevu wa shilingi za Kenya 42 milioni inazodaiwa ada za udalali ambazo zililipwa kwa kampuni ya udalali isiyo na leseni zinazohusiana na mashindano ya CHAN, mwaka uliopita.





