Mourinho aachana ghafla na Roma
Sisti Herman
January 16, 2024
Share :
Klabu ya AS Roma ya ligi kuu ya soka nchini Italia imethibitisha kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba na kocha wao mkuu Jose Mourinho raia wa Ureno, leo msimu ukiwa katikati.
“Tunamtakia kila la kheri Mourinho kwenye majukumu yake mengine kwenye ukurasa mpya wa maisha” ilieleza sehemu ya taarifa kwa umma wakati ikimuaga.
Wapi uelekeo mpya wa Mourinho, tutakujuza.