Mourinho afunguka alivyomshawishi Vini Jr kusalia Real Madrid.
Joyce Shedrack
August 20, 2026
Share :
Kocha Real Madrid José Mourinho amefichua kuwa aliwahi kuzungumza moja kwa moja na nyota wa Real Madrid Vinícius Jr na kumshauri asiondoke katika klabu hiyo.

Mourinho amesema alimuuliza Vinícius kuhusu klabu ambayo angependa kwenda iwapo angeamua kuondoka Real Madrid na alimkumbusha Mbrazil huyo kuwa maisha yake ya soka kwa kiwango cha juu yamejikita zaidi Real Madrid.
“Nilimpigia Vini na kumwambia, Vini, unataka kwenda wapi? Unaijua Real Madrid pekee. Lakini ukiondoka, ndipo utajua Real Madrid ni nini. Usiondoke,” Mourinho.
Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid aliongeza kuwa, kwa mtazamo wake, kuondoka katika klabu hiyo “haifai”akisisitiza kwamba Vinícius anapaswa kuendelea kubaki Santiago Bernabéu huku akisisitiza wazi kuwa nyota huyo anaipenda sana Real Madrid.





