Mourinho afupisha likizo za wachezaji, awaita kambini
Eric Buyanza
June 27, 2024
Share :
Ikiwa ni mwezi mmoja tu tangu kutangazwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Fenerbahce ya ligi kuu Uturuki, Jose Mourinho tayari amewaita kambini wachezaji wa timu hiyo waliopo likizo wale wasiotumikia timu zao za Taifa kwenye mashindano makubwa kama kombe la mataifa Ulaya (EURO) na Amerika (Copa America).
Mourinho ameanza programu za mazoezi ikiwa ni siku 28 tu tangu msimu wa mashindao uishe huku wachezaji wengi wakiwa kwenye amjuku ya timu za Taifa.
Wengi wamepongeza hatua hiyo ikiwa inaenda sambamba na kuwahi kwa msimu wa mashindano kwa Fenerbahce kwani mwishoni mwa mwezi Julai wataanza msimu wa mashindano kwa mechi za kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) msimu ujao.
Fenerbahce walimaliza msimu uliopita wa ligi kuu Uturuki wakiwa nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Galatasaray huku kimataifa wakiondolewa kwenye hatua ya robo fainali ya UEFA Europa League na Olympiakos ambao baadae walikuja kutwaa taji hilo.