Mourinho ahitaji Pongezi Hispania kuwa Bingwa EURO 2024
Sisti Herman
July 16, 2024
Share :
Baada ya timu ya Taifa Hispania kuibuka mabingwa wa kombe la Mataifa Ulaya (EURO 2024) kwa kuwachapa Uingereza kwenye mchezo wa fainali, aliyekuwa kocha wa klabu za Real Madrid na Barcelona kama kocha msaidizi Jose Mourinho amesema amechangia kwa kiasi timu hiyo kuwa mabingwa kwasababu baadhi ya wachezaji waliwapa taji yeye alichangia kuwapa mechi za kwanza wakiwa vijana wadogo.
"Pongezi kwa Nacho Fernandez ambaye pia ni mshindi wa UEFA Chamipons League, Alvaro Morata nahodha wa kikosi,Dani Carvajal kwa kutwaa Ubingwa Euro 2024, pongezi kwangu kocha niliyewapa fursa kucheza mechi zao za kwanza, Pia Pongezi kwa kocha De la Fuente" alisema Mourinho kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Hispania walitwaa Ubingwa huo kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Uingereza, shukrani kwa mabao ya Nico Williams na Mikel Oyarzabal.