MOURINHO ALIPUKA: "Ukizingua, hutakaa hata benchi, utabaki nyumbani"
Eric Buyanza
October 10, 2026
Share :

Kocha mkuu wa Real Madrid, José Mourinho, ameweka wazi msimamo wake mkali kuhusu nidhamu kikosini, akitishia kuwa mchezaji yeyote atakayeshindwa kutimiza wajibu wake basi hatapewa nafasi hata ya kukaa benchi, bali ataachwa nyumbani.
Mourinho alitoa onyo hilo kali jana tarehe 9 Oktoba 2026 wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa LaLiga dhidi ya Villarreal.
"Naahidi kwamba ikiwa mchezaji wa Real Madrid hatatenda kama mchezaji wa Real Madrid na akashindwa kutimiza wajibu wake kama mchezaji, hautamwona mchezaji huyo hata kwenye benchi. Hautapata hata nafasi ya kumzomea kwa sababu atakuwa ameachwa nyumbani. Sitampa nafasi ya kukaa benchi." alisema Mourinho.





