pmbet

Mourinho amenipa uhuru wa kutamba - Bellingham

Eric Buyanza

August 31, 2026
Share :

Kiungo wa kimataifa wa England, Jude Bellingham, amemwagia sifa kocha wake mpya José Mourinho kwa kubadilisha majukumu yake uwanjani, akidai kuwa mfumo wa sasa unampa "uhuru mkubwa wa kuzurura uwanjani" na unamfanya aonyeshe uwezo wake halisi.

 

Bellingham aliyasema hayo kupitia chaneli rasmi ya klabu ya Real Madrid TV kufuatia ushindi mnono wa 4-0 dhidi ya Málaga kwenye uwanja wa Santiago Bernabéu, matokeo yaliyomwezesha Mourinho kuandika rekodi mpya ya kushinda mechi tatu za kwanza za ligi mfululizo tangu arejee klabuni hapo msimu huu wa 2026/27.
 

"Najisikia mwenye uhuru mkubwa tena, uhuru wa kuamua wakati gani nishuke chini kusaidia timu, wakati gani nisogee mbele, au wakati gani nifanye mashambulizi ya kushtukiza ndani ya boksi la wapinzani. Nafikiri hii ndiyo nafasi bora zaidi kwangu kwani inaniruhusu kuonyesha vipaji vyangu vyote. Ninamshukuru sana kocha kwa kuniamini na kunipa nafasi ya kucheza hivi."

 

Katika misimu iliyopita, Bellingham mara nyingi alilazimika kushuka chini kabisa kusaidia ulinzi upande wa kushoto, jambo ambalo liliondoa makali yake ya ushambuliaji.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet