Mourinho aomba usajili wa kiungo mwenye sifa za Modric
Eric Buyanza
June 25, 2026
Share :
Kocha mkuu wa Real Madrid, Jose Mourinho, ameripotiwa kuendelea kushinikiza kuongezwa kwa wachezaji wengine wawili licha ya klabu hiyo kufikia makubaliano ya kuwasajili nyota kadhaa wakubwa.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Brahima Konaté, Denzel Dumfries, Marc Cucurella na Bernardo Silva tayari wamejiunga na Real Madrid, na wanatarajiwa kutua rasmi katika dimba la Santiago Bernabéu mara baada ya kumaliza majukumu yao kwenye Kombe la Dunia la 2026.
Hata hivyo, Mourinho bado anaamini kikosi chake kinahitaji kuimarishwa zaidi. Kwa mujibu wa gazeti la Marca, kocha huyo ameiomba menejimenti ya Real Madrid kufanya usajili mwingine wa beki wa kati atakayeshirikiana na Konaté katika safu ya ulinzi.
Mbali na hilo, Mourinho pia anataka kusajiliwa kiungo mwenye sifa zinazofanana na zile za nguli wa klabu hiyo, Luka Modrić.
Inadaiwa kuwa anatafuta mchezaji mwenye uwezo wa kutawala mchezo, kutoa pasi za ubunifu na kuiongoza timu katikati ya uwanja kama alivyokuwa akifanya Modrić kwa miaka mingi akiwa Real Madrid.

Hatua hiyo inaonyesha dhamira ya Mourinho ya kuhakikisha Real Madrid inakuwa na kikosi chenye ubora kwa ajili ya kupigania mataji makubwa msimu ujao.





