pmbet

Mourinho asema, “Sijafanya mawasiliano yoyote na Real Madrid"

Eric Buyanza

May 11, 2026
Share :

Kocha wa Benfica, Jose Mourinho, amesisitiza kwamba hajawasiliana na Real Madrid kuhusu kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo.
 

Mourinho alisema haya katika mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya mechi ya Benfica dhidi ya Braga siku ya Jumapili.

 

Kumbuka Mreno huyo amekuwa akihusishwa pakubwa na kazi ya ukocha wa Real Madrid katika siku za karibuni.

 

Real Madrid bado inatafuta kocha wa kudumu baada ya kumfukuza Xabi Alonso miezi michache iliyopita na walimteua Alvaro Arbeloa kama kocha wa muda hadi mwisho wa msimu.

 

Hata hivyo, alipoulizwa iwapo Real Madrid imewasiliana naye, Mourinho alisema, “Sijafanya mawasiliano yoyote na uongozi wa klabu ya Real Madrid."

"Sitajadili mambo haya na mtu yeyote. Sitazungumzia hilo" alisema.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet