Mourinho aweka hadharani kikosi kitakachocheza leo
Eric Buyanza
August 8, 2026
Share :

Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho, ametaja kikosi chake kitakachokabiliana na klabu ya Ferencvaros katika mechi ya kirafiki ya maandalizi ya msimu mpya.
Timu hizo zitakutana jijini Budapest nchini Hungary kwenye uwanja wa Ferencváros Stadion leo saa 2 usiku.
Kikosi cha Mourinho kinaingia katika mchezo huo baada ya kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Fiorentina katika mechi yao ya mwisho ya kirafiki.
Hata hivyo, Mourinho ameamua kuwajumuisha wachezaji kama Bernardo Silva, Vinicius Junior, Endrick na Arda Guler katika kikosi chake kitakachocheza dhidi ya Ferencvaros.
Kikosi cha Real Madrid dhidi ya Ferencvaros:
MAKIPA:
Lunin, Sergio Mestre, na Javi Navarro.
WALINZI:
Trent, Carreras, Rudiger, Huijsen, Dumfries, Joan Martínez, Lamini, na Mario Rivas.
VIUNGO:
Camavinga, Valverde, Arda Guler, Bernardo Silva, Cestero, Lacosta, na Alexis Ciria.
WASHAMBULIAJI:
Vinicius Junior, Brahim, Endrick, Carlos Espi, na Daniel Yanez.





