pmbet

Mourinho hatimaye akubali dili la kuinoa Real Madrid

Eric Buyanza

May 16, 2026
Share :

Meneja wa Benfica, Jose Mourinho, hatimaye amefikia makubaliano na Real Madrid kurejea katika klabu hiyo ya LaLiga.

 

Kulingana na gazeti la Marca, Mourinho anatazamiwa kuiaga Benfica mwishoni mwa msimu huu.

 

Madrid itailipa Benfica ada ya takriban Euro milioni 3 ili kumwachilia kocha huyo mwenye umri wa miaka 63 kutoka kwa mkataba wake wa sasa.

 

Mourinho mwenyewe alifichua kwamba alikataa ofa mpya kutoka kwa Benfica, alipokuwa akijiandaa kuinoa Madrid.

 

Kocha mkuu wa sasa, Alvaro Arbeloa, alichukua tu nafasi ya Xabi Alonso mwezi Januari na anatazamiwa kuondoka baada ya mechi ya mwisho ya ligi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet