pmbet

Mourinho kuuhamisha ukuta wa Man Utd kwenda Uturuki

Eric Buyanza

June 17, 2024
Share :

Meneja wa Klabu ya Fenerbahce ya Uturuki, Jose Mourinho ameripotiwa kuitamani huduma ya beki wa Manchester United, Victor Lindelof ili kuimarisha kikosi chake.

Mourinho anataka kumuona mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden akicheza kwenye Uwanja wa Sukru Saracoglu unaomilikiwa na Fenerbahce.

Mourinho ambaye amepata mafanikio makubwa kama mwalimu akiwa nchini Ureno, Uingereza, Italia na Hispania, sasa anajaribu kutaka kuacha alama yake kwenye soka la Uturuki.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet