Moyo wako unadunda mara 101,000 kwa siku, husukuma damu lita milioni 400!
Eric Buyanza
January 18, 2024
Share :
Moyo unadunda mara 101,000 kwa siku. Moyo wa mwanadamu unasukuma damu mwili mzima, ikisambaza hewa safi, virutubisho na kuondoa hewa chafu na uchafu mwingine. Ukiwa umepumzika moyo wako unadunda mara 60 mpaka 100 kwa dakika moja.
Kwa mujibu wa mtandao wa Wonderpolis, ukikimbia au kucheza soka kwa dakika 90, au mazoezi mengine, moyo wako hudunda haraka zaidi kwasababu inabidi kusukuma damu haraka zaidi ili kufikisha hewa ya oksijeni pamoja na virutubisho vinavyohitajika katika seli ili mazoezi yafanyike.
Kwa mujibu wa Revive Functional Medicine Center, katika maisha yako yote, moyo utakuwa umesukuma lita milioni 400 (800 Million pints) za damu.
Kama moyo wako unadunda kwa wastani mara 80 kwa dakika, basi kwa saa moja utakuwa umedunda mara 4,800. Kwa siku ni mara 115,200 na kwa mwaka mara 42,048,000. Na kama utaishi miaka 80, moyo utakuwa umedunda mara 3,363,840,000. Fikiria jinsi msuli huo ulivyo na nguvu na kazi kubwa.