pmbet

Mpango awagusa wanawake na watoto salamu za X-Mass

Sisti Herman

December 25, 2023
Share :

Makamu wa Rais Dk Philip Mpango amewaasa Watanzania kuendelea kupinga aina zote za ukatili kwa wanawake na watoto huku akisisitiza kuwapa watoto malezi bora kwa kuwaongoza katika kumjua Mungu, kuwafundisha uzalendo na kufanya kazi kwa bidii, kuwaongoza katika kuipenda nchi na kuitumikia wakiwa raia na baadae kuwa viongozi waadilifu.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumatatu Desemba 25, 2025 baada ya yeye na mkewe mama Mbonimpaye Mpango kuuungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma katika ibada ya Sikukuu ya Krismasi. Ibada hiyo imeongozwa na Paroko wa Parokia hiyo Padre Emmanuel Mtambo.

Akitoa salamu za Sikukuu ya Krismasi kupitia kwa waumini hao, Dk Mpango pia amewasihi Watanzania kusheherekea sikukuu kwa amani na utulivu pamoja na kujitoa kusaidia wale wasio na uwezo wakiwemo yatima.

Aidha amewashihi waumini na viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa ili amani iweze kudumu na kuepushwa na mafarakano huku akiwaasa kujiandaa ili kushiriki vema uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024 pamoja na kuliombea taifa kupata viongozi waliobora.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet