pmbet

Mpanzu haendi Simba kwasababu nawadai, anaenda Ulaya - Wakala

Sisti Herman

July 24, 2024
Share :

Wakala wa winga wa klabu ya AS Vita ya nchini Congo DR Ellie Mpanzu anayefahamika kwa jina la Papida amesema ni ngumu kwa mchezaji huyo kujiunga jna tumu hiyo kwani tayari amepata ofa kubwa zaidi barani Ulaya.

“Tofauti ya Simba na Yanga ni kuwa Yanga wanapotaka Mchezaji unawasiliana na Mtu mmoja tu ila Simba watu ni wengi sana kwa dili moja, mara Salim, mara Mulamu mara Magori na pia walikuja kwa kuchelewa sana kuhusu kumtaka Mchezaji wangu Ellie Mpanzu"

"Hata hivyo hawezi kwenda Simba anaenda Ulaya, lakini nilishawaambia Simba ipo siku watanitafuta, nitawapa Wachezaji wakishanilipa pesa yangu dola 5,000 kuna dili tulifanya na wanajua”

“Simba hawana sera nzuri ya kutafuta Wachezaji, wanapaswa kuelewa Congo ama Afrika ina Wachezaji wengi wazuri sana, ila unapaswa kuwachukua wakiwa na umri mdogo niliwapa ushauri wachukue Wachezaji wa miaka 15-17 wapikwe kwenye mifumo yao watakuja kuwa wazuri sana baadae, hawataki wanataka wachezaji ambao wameshakomaa hiyo sio sera nzuri, kwa Tanzania Simba ni timu yangu, mimi sishabikii Yanga”

Hizo ni nukuu za Wakala Papida ambaye anasimamia dili za uhamisho za Ellie Mpanzu alipozungumza na Bongo FM.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet