"Mpanzu ni mali halali ya Simba anayemtaka aje mezani" Try Again.
Joyce Shedrack
May 13, 2025
Share :
Baada ya kuibuka kwa tetesi nyingi zinazomhusu mchezaji wa Simba raia wa DR Congo Ellie Mpanzu kuhusu kuondoka mitaa ya msimbazi msimu ujao na kuibukia mitaa ya Jangwani Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Simba Salim Abdallah Muhene 'Try Again' amekanusha tetesi hizo na kusema nyot huyo ni mali halali ya Simba.

Hapo awali tetesi ziliibuka kuwa viongozi wa Yanga wamewasiliana na klabu ya AS Vita ili kupata huduma ya nyota huyo na tayari wamemalizana na viongozi hao kwa kufanya biashara ya mchezaji huo kutokana na kuwa kwa mkopo ndani ya klabu ya Simba.
Taarifa hizo zilikuwa za uongo kwa sababu mchezaji huyo hakuwa mchezaji halali wa As Vita na Simba walimnunua moja kwa moja kutoka katika klabu yake ya AJ Vainqueur inayoshiriki ligi daraja la tatu DR Congo.
"Elie Mpanzu sisi tumemsajili kwa miaka miwili tena sio miaka miwili tu ni miaka miwili na nusu, pia watu wajue sisi hatujamsajili Elie Mpanzu kutoka AS VITA CLUB sisi tumemsajili kutoka kwenye timu yake inayommliki tena haichezi ligi kuu nahisi inacheza ligi daraja la kwanza ama la pili Congo, Mpanzu mchezaji wetu halali hivyo anayemtaka aje mezani awake pesa kama anazo."- Salim Abdallah Muhene (@salim_tryagain ).