MPASUKO UKRAINE: Fedorov amtolea uvivu Zelensky, ataka uchaguzi ufanyike
Eric Buyanza
August 19, 2026
Share :

Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Ukraine, Mykhailo Fedorov, ametoa wito wa kuitishwa kwa uchaguzi mkuu nchini humo wakati huu wa vita.
Kupitia ujumbe wa video aliopost kwenye mtandao wa YouTube mnamo Jumanne, Agosti 18, 2026, Fedorov mwenye umri wa miaka 35 ametoa changamoto kwa Serikali ya Rais Volodymyr Zelensky akitaka utaratibu wa kisheria na salama upatikane ili kurudisha demokrasia, akisisitiza kuwa “demokrasia haiwezi kushikiliwa mateka na Urusi.”
Fedorov ameeleza kuwa Ukraine inakabiliwa na mfumo mbovu wa utawala na rushwa inayorudisha nyuma juhudi za vita.
Fedorov aliondolewa ghafla kwenye nafasi yake ya Uwaziri wa Ulinzi mwezi Julai 2026 baada ya kutofautiana na viongozi wa kijeshi, hatua iliyosababisha maandamano makubwa ya wananchi wakimpinga Rais Zelensky.
Amesema kama vita vitachukua miaka mingi, si sawa kwa Urusi kuamua ni lini Waukraine wanaweza kuchagua viongozi wao.
Chini ya sheria za sasa za Ukraine na hali ya hatari ya kijeshi (martial law) iliyowekwa tangu Urusi ilipovamia nchi hiyo mwaka 2022, uchaguzi umezuiwa kisheria. Hata hivyo, Fedorov anataka kutafutwe njia mbadala ya kufanikisha uchaguzi huo ili wananchi wapate haki yao ya kidemokrasia.





