Mpenzi wa Justine Bieber akanusha kufurahia penzi la Selena Gomez mpenzi wake kuvunjika.
Joyce Shedrack
March 10, 2025
Share :
Muwakilishi wa Hailey Bieber's ambaye ni mpenzi wa Justin Bieber amefuta uvumi uliokuwa ukisambaa kuwa Hailey alishawahi ku 'like' ujumbe wa video uliokuwa una-diss penzi la Selena Gomez na mpenzi wake Benny Blanco.
Muwakilishi huyo amedai kuwa story hiyo ilianzishwa na watengeneza maudhui kupitia mtandao wa TikTok wakihitaji kumchafua Hailey kutokana na uhusiano ambao upo baina ya Selena Gomez na Hailey Bieber.
Selena na Hailey wamekuwa na mahusiano ambayo siyo mazuri kutokana na wote kuwa na mahusiano na Justin Bieber kwa nyakati tofauti Hailey alianza mahusiano na Justin 2018 huku Selena akiweka mahusiano yake na Blenny Blanco 2023 na kuvalishana pete ya uchumba disemba mwaka jana.