pmbet

Mpina kuwapeleka Spika na Bashe Mahakamani

Sisti Herman

June 30, 2024
Share :

Mbunge Mbunge wa Kisesa (CCM) Luhaga Mpina ambaye anatumikia adhabu ya kutohudhuria vikao 15 vya Bunge, amesema anatarajia kupeleka mahakamani malalamiko yake ya kuondolewa Bungeni kwa kile alichodai kuwa kuna uonevu na kutokutendewa haki na Spika wa Bunge, Tulia Ackson.

Akizungumza alipokutana na Wanahabari jana Juni 29, 2024, Mpina ameongeza kuwa atawafikisha Mahakamani Waziri Bashe na Bodi ya Sukari chini ya lbara ya 26 na 27 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kitendo cha kutoa idhini ya vibali vya kuagiza sukari kinyume cha Sheria na kulisababishia Taifa hili hasara kubwa.

Vilevile Mpina amesema atayafikisha Mahakamani makampuni yote yaliyojihusisha na uingizaji wa sukari Nchini kinyume cha Sheria.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet