Mpole atua kwenye mikono ya Mabosi Yanga
Sisti Herman
June 26, 2024
Share :
Klabu ya Yanga inatajwa kuwania saini ya mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2021/22 George Mpole aliyemaliza mkataba wake akiwa na FC Saint Eloi ya ligi kuu ya Congo DR.
Mpole ambaye aliibuka mfungaji bora kwa kufunga magoli 17 juu ya aliyekuwa mshambualiaji wa Yanga Fiston Mayele aliyemaliza na magoli 16, msimu huu ameshindwa kutamba kwenye ligi ya Congo kiasi cha kufikia hatua ya kutoongeza mkataba mpya nchini humo.