Mr Ibu kuzikwa baada ya miezi mitatu, Kamati ya mazishi yaomba msaada
Sisti Herman
June 3, 2024
Share :
Baada ya kutangaza tarehe ya mazishi ya mwigizaji kutoka Nigeria Mr Ibu, mwenyekiti aliyeteuliwa kusimamia mazishi ya mwigizaji huyo Monday Diamond A. JP (Odoziobodo) ametoa walaka wa kuiomba serikali na wadau mbalimbali kuchangia fedha kwa ajili ya mazishi hayo.
Kufuatia na barua hiyo iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Kamati Kuu Diamond, katibu Ijele, na Rais wa Chama cha Waigizaji cha Nigeria, Emeka Rollas imelenga kuomba msaada wa kifedha ili kusaidi kukamilisha mazishi hayo kama yalivyopangwa.
Ikumbukwe kuwa Mr Ibu (62) amefariki dunia Machi 2, 2024 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Evercare iliyopo nchini Nigeria, na anatarajiwa kuzikwa Juni 28, 2024 katika mji aliozaliwa wa Amuri, katika eneo la serikali ya mtaa wa Nkanu Magharibi katika Jimbo la Enugu.
Mazishi ya mwigizaji huyo yanapangwa kuwa ya kihistoria kwa kuwepo kwa sherehe ya siku tano ambapo hafla hiyo itaanza Juni, 25 kutakuwa na mechi maalumu, June 26 Usiku wa Mr Ibu kutakuwa na mishumaa pamoja na kupata burudani ya moja kwa moja.
June 27 kutakuwa na ibada maalumu nyumbani kwao huko Eziokwe Amuri, ibada ya mazishi ikifanyika June 28 na sherehe hizo zitatamatika Jumapili June 30 ambapo familia itatoa shukrani kwa kanisa, marafiki na watu wengine waliohudhuria katika hafla zote za siku tano.
Mr Ibu watu wengi walimtambua kupitia filamu zake kama The Collaborator, My Chop Money na nyingine nyingi akiwa na Aki na Ukwa.