Mrithi wa Bocco Simba apewa 'Thank You' Msimbazi.
Joyce Shedrack
June 19, 2024
Share :
Klabu ya Simba imeachana na mshambuliaji wake Shaaban Idd Chilunda aliyedumu kwenye timu huyo kwa msimu mmoja pekee akisajiliwa kutokea kwa matajiri wa jijini la Dar es Salaam Azam Fc.
Chilunda ambaye hakuwa na msimu mzuri tangu ajiunge na klabu hiyo hakupata nafasi kubwa ya kucheza kwenye klabu ya Simba na baadae Simba ilimtoa kwa mkopo kwenda klabu ya KMC ili kupata nafasi zaidi ya kucheza.
Mshambuliaji huyo mzawa anakuwa mchezaji wa tatu kufikiwa na ‘Thank You’ zinaloendelea ndani ya kikosi cha mnyama kwa ajili ya maboresho ya timu hiyo kuelekea msimu ujao.
Wachezaji wengine walioagwa ni Saido Ntibanzonkiza pamoja na John Rafael Bocco.
Taarifa nyingine kuhusu mchezaji atakayefata itatolewa na klabu hiyo leo saa 11 jioni.