Mrithi wa Inonga Simba huyu hapa
Sisti Herman
June 26, 2024
Share :
Klabu ya Simba inahusishwa kuwania saini ya beki wa kati wa timu ya Taifa ya Congo DR anayecheza Vålerenga IF ya Norway kwaajili ya kuziba pengo la aliyekuwa beki wao wa kati Henock Inonga Baka aliyeuzwa ASFAR ya Morocco.
Beki huyo ambaye pia amecheza Capetown City Fc ya Afrika kusini na FC Saint Eloi ya Congo anaweza kujiunga Simba kama watafikia makubaliano na atakuwa beki wa pili kusajiliwa baada ya Lameck Lawi kutoka Coastal Union ya Tanga.