Mrithi wa Saido atua Dar kimyakimya kujiunga na Simba
Sisti Herman
June 26, 2024
Share :
Aliyekuwa Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Power Dynamos, Joshua Mutale anatajwa na vyombpo mbalimbali vya Zambia kuwasili jijini Dar es Salaam kwaajili ya kukamilisha taratibu za kujiunga na klabu ya Simba.
Mutale anayetajwa kukubali kusaini dili la kujiunga Simba kwa mkataba wa miaka mitatu kama mbadala wa kiungo mshamliaji aliyeondoka Saido Ntibanzokiza ambaye alikuwa mfungaji bora wa Simba kwa miaka miwili mfululizo.
Mutale pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Zambia.