Mr.P wa P Square abadilisha tarehe yake ya kuzaliwa ili asifanane na pacha wake.
Joyce Shedrack
April 21, 2026
Share :
Msanii kutoka Nchini Nigeria, Peter Okoye maarufu kama Mr P, ametangaza rasmi kubadili tarehe ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ili isifanane na pacha wake Paul Okeye maarufu kama RudeBoy.
Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa X (zamani Twitter), Mr P amesema kuwa kuanzia sasa hatasherehekea tena siku yake ya kuzaliwa tarehe 18 Novemba, ambayo ni tarehe moja na pacha wake na hatapokea ujumbe wala zawadi zozote siku hiyo.
Aidha, msanii huyo ameeleza kuwa siku yake ya kuzaliwa itakuwa
ikiadhimishwa tarehe 30 Novemba kuanzia sasa akisisitiza kuwa huo ni uamuzi binafsi na ameomba mashabiki, familia na marafiki kuheshimu uamuzi huo.





