pmbet

Msajili wa vyama vya michezo akabidhi rasmi katiba mpya ya Simba kwa uongozi.

Joyce Shedrack

February 18, 2026
Share :

Msajili wa vyama vya michezo Abel Ngilangwa ametangaza kuwa ameshakabidhi Katiba Mpya ya Simba kwa Uongozi wa Klabu hiyo.

Maboresho yaliyofanywa kwenye Katiba ya Klabu ya Simba na kuidhinishwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za usajili wa vyama vya michezo yanalenga kuimarisha muundo wa uendeshaji, umiliki na usimamizi wa Klabu ili kuwezesha uwekezaji na uwajibikaji wa taasisi zake.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Katiba imeweka tafsiri sahihi ya Simba Sports Club Company Limited kama kampuni iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Makampuni, itakayoshughulikia shughuli za kibiashara na kiutendaji za Klabu, huku umiliki wa hisa ukiwa wa ubia kati ya Baraza la Wadhamini kwa niaba ya wanachama na wawekezaji kwa mujibu wa sheria na maamuzi ya Mkutano Mkuu.

 

Aidha, imeainishwa wazi kuwa hisa za Klabu zitamilikiwa kupitia Baraza la Wadhamini kwa niaba ya wanachama.
 

Maboresho hayo pia yameimarisha muundo wa Baraza la Wadhamini kwa kuweka idadi ya wajumbe kati ya watano na saba, wenye jukumu la kumiliki na kusimamia mali za Klabu kwa niaba ya wanachama, huku Mkutano Mkuu ukiendelea kuwa chombo chenye mamlaka ya kuthibitisha uteuzi na kumuondoa mjumbe wa Baraza hilo.
 

Serikali imeeleza kuwa maboresho hayo ni ya kuboresha mfumo uliopo kwa kuendana na maamuzi yaliyokwisha kupitishwa na Mkutano Mkuu, bila kuanzisha mfumo mpya wala kubadili maamuzi ya wanachama.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet