Msako mkali waja kwa wauza mafuta kwenye vidumu
Eric Buyanza
May 9, 2024
Share :
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA ) Kanda ya Magharibi, imetangaza kuanza msako mkali wa kuwakamata wafanyabiashara wanaouza mafuta ya petroli/dizeli kwenye vidumu na mapipa jambo ambalo linakiuka sheria na kuhatarisha maisha ya wananchi.
Msako huo umetangazwa na Meneja wa EWURA wa Kanda hiyo, Walter Chirstopher, wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo alisema wafanyabiashara hao siku zao zinahesabika na wakikamatwa watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kukiuka sheria za mamlaka hiyo.
“Sheria ya mafuta ya mwaka 2015 kifungu cha 131 inasema mtu yoyote haruhusiwi kuuza mafuta hayo bila kuwa na leseni kutoka EWURA,” amesema na kufafanua kuwa: “ Masharti ya EWURA mfanyabiashara anayotakiwa kuyatimiza ni kuwa na leseni na kujenga kituo cha mafuta."