pmbet

Msako wa kuwasaka wazee wasiotahiriwa waibua mjadala mzito

Eric Buyanza

October 27, 2026
Share :

Baraza la Wazee la Jamii za Mlima Kenya, limeanzisha msako wa siku 100 wa kubaini wazee wa jamii za Gema ambao hawajatahiriwa, hatua inayozua mjadala kuhusu faragha na mila.
 

Mlezi wa kitaifa wa baraza hilo, Kung’u Muigai, alisema zoezi hilo linawalenga wazee wote 3,674 waliosajiliwa kuendesha shughuli za kitamaduni.
 

Alisema kila mzee atalazimika kuthibitisha kuwa ametahiriwa, huku zoezi hilo likifanywa kwa hiari na kwa faragha katika madhabahu ya kitamaduni.

 

Muigai alisema suala hilo lilijadiliwa katika mkutano wa wazee 63 uliofanyika Kaunti ya Kiambu Septemba 28, baada ya kile alichokitaja kuwa mgogoro wa kitamaduni uliosababishwa na migawanyiko na tamaa.

 

Alisema tangu 2010, visa 340 vya wazee ambao hawajatahiriwa vimeripotiwa, huku 146 vikigunduliwa baada ya vifo vyao.

 

Wazee watakaokataa kushiriki zoezi hilo wataondolewa kwenye sajili ya wanaoruhusiwa kutekeleza majukumu ya kitamaduni.
 

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Kikuyu, Wachira Kiago, alisema tohara ni sehemu muhimu ya utambulisho wa jamii, akisisitiza kuwa baraza linapendelea mazungumzo badala ya vurugu.

 

Muigai alisema baadhi ya wazee wamefichuliwa baada ya kugombana na wake zao, huku wengine wakigunduliwa walipolazwa hospitalini.
 

Bwana Joseph Kaguthi, mratibu wa baraza linalowakutanisha wazee wa Gema na viongozi wa dini, alisema mwanaume ambaye hajatahiriwa haruhusiwi kushiriki katika mikutano ya wazee, kufanya maamuzi ya kitamaduni au kutekeleza baadhi ya mila.

 

Chanzo: TaifaLeo

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet