Msala wa Diddy wamkuta mtoto wake
Sisti Herman
April 3, 2024
Share :
Mwendelezo wa sakata la tuhuma za unyanyasaji wa kingono la rapa P Diddy, taarifa mpya ni kuwa mtoto wa rapa 'Christian' maarufu kama King Combs anaungana na baba yake kwenye tuhuma za unyanyasaji wa kingono baada ya mwanamke mmoja ambaye hajawekwa wazi kudai alinyanyaswa kingono na mtoto wa Diddy.
Kwa mujibu wa Tyrone Blackburn ambaye ni mwanasheria anayewawakilisha wanawake kadhaa wanaomtuhumu Diddy kwa vitendo vya unyanyasaji amesema kwamba kesi hiyo bado haijafunguliwa lakini ipo mbioni kuwasilishwa mahakamani na Diddy tayari analifahamu hilo.
Christian amewahi kuhusishwa kuwa kwenye mahusiano na wanawake tofauti kama Breah Hicks ambaye alikuwa nae kwa miaka kadhaa na sasa yupo na mwanamitindo Raven Tracy (The Neighborhood Talk).