Msanii wa FM Academia afariki akitumbuiza jukwaani
Sisti Herman
April 7, 2024
Share :
Kiongozi wa bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia Patcho Mwamba amethibitisha kifo cha mwimbaji maarufu wa bendi hiyo na mkongwe wa muziki wa dansi Malu Stonch kilichotokea jana Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Inasemekana Malu alianguka ghafla jukwaani wakati bendi hiyo ikitumbuiza kwenye ukumbi wa Target uliopo Mbezi Beach kabla ya kukimbizwa hospitali ambapo iligundulika kuwa amefariki dunia.
Enzi za uhai wake Malu alitamba kwenye bendi kama Stono Musica na Stono Mayasica.