pmbet

Msauzi awa kocha Mkuu Singida

Sisti Herman

January 1, 2024
Share :

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Singida Fountain Gate, Olebile Sikwane raia wa Zimbabwe amesema kwa sasa timu hiyo itakuwa chini ya Kocha Mkuu, Thabo Senong raia wa Afrika Kusini hadi mwisho wa msimu baada ya kikosi hicho kuachana na Mbrazili, Ricardo Ferreira.


Singida leo inashuka uwanjani kuvaana na APR ikiwa ni mechi ya pili baada ya awali kuifunga JKU mabao 4-1. Akizungumza, Olebile alisema hawatofanya maamuzi ya haraka kutafuta kocha mwingine na badala yake wameona ni vyema kumpa nafasi hiyo Senong wakiamini ana uzoefu mkubwa wa kutosha na amekuwa na maelewano mazuri na wachezaji.

“Tunajifunza kutokana na makosa, tumekaa sisi kama viongozi na kuona sio muda tena wa kufanya haraka za kumpata kocha mpya kwa sasa, tumeridhika na uwezo wake hivyo tutampa ushirikiano wa kutosha hadi tutakapoamua vinginevyo,” alisema.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet