Msemo wa 'Mpira huo' wamfikia admin wa Liverpool ya Uingereza
Eric Buyanza
October 22, 2026
Share :
Usemi wa 'MPIRA HUO' unaopendwa kutumiwa na mshambuliaji wa timu za Mtaani ‘Ndondo’ Mashaka Pogba, umepenya hadi kufika nchini Uingereza katika klabu ya Liverpool.
Msemo huo umetumika katika ukurasa rasmi wa Liverpool na kuwekwa picha ya mlinzi Ronald Araujo ambaye juzi alikuwa sehemu ya wafungaji waliofunga bao katika ushindi wa 4-3 walioupata Liverpool dhidi ya Villareal.
Katika machapisho mengi ya Mashaka Pogba katika ukurasa wake wa Instagram amekuwa akiandika usemi huo ambao sasa umepasua anga la kimataifa.






