Mshahara wa Mbappe Madrid ni Nomaa
Sisti Herman
February 19, 2024
Share :
Mara baada ya kuaga kunako mabingwa wa ligi kuu Ufaransa PSG, mshambualiaji hatari wa klabu hiyo anayedaiwa kuwa kwenye hatua za mwisho kujiunga na Real Madrid Kylian Mbappe inasemekana kuwa atasaini mkataba wa miaka mitatu na mabingwa hao mara nyingi zaidi wa ligi ya mabingwa Ulaya.
Wadadisi wa masuala ya usajili kutoka jarida la Marca la nchini Hispaniola wameweka wazi kuwa mshambuliaji huyo mshindi wa kombe la dunia atasaini mkataba wa miaka mitatu hadi 2029 na kulipwa kiasi cha Euro milioni 15-20 kwa msimu huku akikunja kitita cha Euro milioni 50 kama bonasi ikumbukwe anajiunga Madrid kama mchezaji huru.
Wadadisi hao pia wamesema utambulisho wa mchezaji huyo utaambatana na ufunguzi wa uwanja wa Santiago Bernabeu baada ya kufanyiwa maboresho makubwa kwa misimu miwili.