Mshahara wa Mfalme Charles kufikia Bilioni 155
Sisti Herman
July 31, 2024
Share :
Mfalme wa Uingereza, Charles Philip Arthur George "Charles III" anatarajiwa kuongezwa kwa mshahara wake ambapo kutakuwa na ongezeko la kufikia mshahara wa Pauni Milioni 45 (sawa na Tsh Bilioni 155.961) kwa Mwaka.
Pia kutakuwa na ongezeko la Ruzuku ya Utawala, kwaajili ya kuhudumia majukumu na gharama rasmi za Familia hiyo ya Kifalme ambayo itapanda kutoka Pauni Milioni 86 (sawa na Tsh bilioni 256.06) ya 2024-25 hadi kufikia Pauni Milioni 132 (sawa na Tsh Bilioni 457.932) mwaka 2025-26, hii ni kutokana na kuongezeka kwa faida kutoka kwa Crown Estate.