pmbet

Msiangalie fedha kama kigezo kuchagua kiongozi - Dkt. Nchimbi

Eric Buyanza

May 31, 2024
Share :

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel Nchimbi, ametoa onyo kwa viongozi wa Chama hicho nchini ngazi zote, kutotumia kigezo cha mtu mwenye fedha nyingi kuwa ndiye anayefaa kuwa kiongozi.

Nchimbi alisema sifa kuu ya kiongozi ni yule mwenye uwezo na utayari wa kuhudumia wananchi.

Hayo yalisemwa Balozi Nchimbi akiwa Mkoani Singida katika mkutano wa ndani uliohusisha viongozi na wanachama wa CCM, mabalozi watendaji wa serikali pamoja na wananchi.

Amesema wakati huu ambao CCM inajiandaa kuingia katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji, Chama kinapaswa kusimamisha wagombea wenye kukubalika kwa uwezo wao wa kutatua changamoto za wananchi.

“Viongozi kataeni kutumika, msichague viongozi kwa sababu ya fedha bali tengenezeni ramani ya kuwapata viongozi bora, mkatae kuyumbishwa, wapimeni watu kwa uwezo wa kuongoza, kuheshimu na pale shida za wananchi zinavyowagusa kwani sifa Kuu ya kiongozi ni kufahamu nafasi wanazotumikia ni kwa ajili ya wananchi." alisema Balozi Nchimbi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet