pmbet

'Msiingize vidole ukeni, mtapata Saratani' – Zuhura

Eric Buyanza

December 22, 2023
Share :

Kunawa kwa kuingiza vidole sehemu za uke, kujifukiza na matumizi ya bidhaa mbali mbali ikiwemo asali kuwekwa ukeni, kuwa na wapenzi wengi, kujamiiana katika umri mdogo na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU).....vyote hivyo vimetajwa kuwa kisababishi kikubwa cha ongezeko kubwa la saratani ya kizazi.
 

Tafiti zinaonesha kuwa wale wanaojisafisha sehemu za uke kwa kujiingiza vidole wako hatarini kwa sababu huwa wanaondoa bakteria walinzi waliopo ukeni. Ukiwaondoa hao bakteria, virusi wanaweza kujibadilisha na kuwa saratani.

Mratibu wa Kitaifa wa Afya ya Mama na Mtoto, Zuhura Mbuguni amesema uke unajisafisha wenyewe kuingiza vitu tofauti ni hatari kwa mwanamke.
 

“Uke unajisafisha wenyewe, kuingiza kitu kisicho cha kawaida kinaharibu bakteria wake wa asili, kuna wanawake wengine wanatabia ya kujiwekea vitu vyenye kemikali kama sabuni mara wengine wanaweka asali, ndimu, pafyumu, kujifukiza ili kuwaridhisha wanaume, vitu hivi vinaua wale bakteria walioko sehemu za uke na vingine husababisha mchubuko, hivi vyote ni hatari kwa mwanamke,”amesema Zuhura

 

Mbali na saratani ya kizazi, madhara mengine wanayoweza kupata wanawake wanaotumia vitu hivyo ni ugumba, kuziba kwa mirija ya uzazi, shambulizi ukeni, maumivu makali chini ya tumbo na maumivu wakati wa kujamiiana.

 Source: HabariLeo
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet