Msijisumbue, Xabi haendi kokote
Sisti Herman
February 13, 2024
Share :
Mkurugenzi wa michezo wa Bayer Leverkursen Simon Rolfes amesema kuwa licha ya kuwa kocha wao mkuu Xabi Alonso kuhitajika na timu vigogo barani Ulaya kama Real Madrid na Liverpool bado wana uhakika wa kuendelea kuwa na kocha huyo pekee ambaye hadi sasa hajapoteza mchezo kwenye mashindano yote msimu huu barani Ulaya.
“Sababu pekee ambayo tuna uhakika nayo ni kuwa kama atakuwa huru, mwenyewe (Xabi) anajua kuwa atakuwa na timu bora zaidi msimu ujao, na uhakika atabaki, kila kitu ni sahihi kwake, namna timu inavyocheza yupo kwenye ubora wake” alisema Mkurugenzi huyo.
Bayer Leverkursen mpaka sasa wamecheza mechi 31 msimuj kwenye michuano yote bila kupoteza mchezo wowote.