pmbet

Msikiti wachomwa moto waumini wakiwa ndani, 11 wafa

Eric Buyanza

May 16, 2024
Share :

Takriban waumini 11 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya mtu mmoja kushambulia msikiti katika jimbo la Kano kaskazini mwa Nigeria, polisi wamesema.
 

Mtu huyo anadaiwa kuumwagia petroli msikiti na kisha kufunga milango kabla ya kuuchoma moto, wakati ndani kukiwa na waumini wapatao 40.
 

Inaelezwa kuwa shambulio hilo lilichochewa na mzozo wa kifamilia kuhusu kugawana urithi.
 

Polisi wanasema wamemkamata mshukiwa mwenye umri wa miaka 38.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet