pmbet

Msimchukulie poa Ayoub - Ahmed Ally

Eric Buyanza

December 11, 2023
Share :

Meneja wa idara ya habari wa klabu ya Simba Ahmed Ally, ametoa taahadhari kwa mashabiki wanaobeza uwezo wa mlinda lango wao raia wa Morocco Ayoub Larkred na kusema ni nyanda mkubwa.
 

"Ayoub ni kipa mkubwa msimchukulie poa, ni kipa mkubwa mno, anaheshimika Morocco, ni mmoja wa makipa mwenye wasifu mkubwa nchini humo, muda unavyozidi kwenda uwezo wake wa kujiamini unazidi kupanda, muda si mrefu wana Simba watafaidi matunda yake" alisema Ahmed kwa kutamba kwenye video aliyochapisha kwenye mtandao wake wa kijamii.
 

Kwenye mchezo dhidi ya Wydad AC, licha ya Simba kupoteza 1-0, nyanda huyo alikuwa kwenye kiwango bora sana akiokoa michomo 5 kati ya mashuti 6 ya Wydad yaliyolenga lango huku mmoja ukiwa mkwaju wa penalti.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet